Mshambuliaji wa zamani wa Yanga Heritier Makambo amesema tetesi zinazomuhusisha na klabu ya Simba ni feki, hazina ukweli wowote
Mcongomani huyo anayekipiga kunako klabu ya Horoya AC amesema alikuwa tayari kurejea Yanga kama sio changamoto ya mkataba wake na Horoya AC
"Hakuna ukweli wowote, kama nisingekuwa na mkataba na Horoya klabu pekee ambayo nilitaka kuja kujiunga nayo ni Yanga, wala sio Simba, " alisema Makambo
Makambo bado ana mkataba wa miaka miwili na Horoya Ac, mwenyewe akisema kuwa hatma yake iko mikononi mwa klabu hiyo kwani timu yoyote wakiwemo waajiri wake wa zamani Yanga, wanapaswa kumalizana na Horoya kuweza kupata huduma yake
ADVERTISE HERE