Mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi amesema anaendelea kupambana kuhakikisha anafanya vizuri na kuisaidia Yanga kufikia malengo yake
Nchimbi ni mmoja wa wachezaji ambao waliongeza uhai kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga pale waliposajiliwa na haikushangaza kuwa miongoni mwa wachezaji 15 waliosalia kutoka kikosi cha msimu uliopita
Msimu ujao Yanga imeweka malengo makubwa ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu, ni jukumu la nyota wote akiwemo Nchimbi kutimiza adhma hiyo
Mwenyewe anasema tangu yuko mtoto msamiati wa kukata tamaa haupo katika kichwa chake hivyo anaamini ataendeleza pale alipoishia msimu uliomalizika
Alimaliza msimu akiwa amefunga mabao sita, mawili akifunga wakati alipojiunga na Yanga
Aliyekuwa kocha wa Yanga Luc Eymael alikuwa akimtumia kama mshambuliaji au winga
Ni mchezaji mwenye juhudi kubwa awapo uwanjani, hakuna shaka ipo nafasi yake katika kampeni ya kuwania ubingwa wa msimu ujao