Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kujiweka sawa tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom unaoanza Septemba 06 2020
Yanga inafanya mazoezi chini ya kocha msaidizi, mtaalam wa viungo Riedoh Berdien wakati wakimsubiri kocha mkuu
Katika wiki hii ya kwanza, wachezaji wamekuwa wakifanya mazoezi wakitokea majumbani kwao, lakini imeelezwa kuwa wataingia rasmi kambini siku ya Jumatatu
Taarifa za ndani zimebainisha kuwa tayari uongozi wa mabingwa hao wa kihistoria umeshampata mrithi wa Luc Eymael kinachosubiriwa ni taratibu za utambulisho tu
Kocha huyo raia wa kigeni pamoja na kocha msaidizi ambaye ni mzawa, wanatarajiwa kuanza kusimamia mazoezi wiki ijayo
ADVERTISE HERE