Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema kutokana na ufinyu wa muda, wamefuta mpango wa kuipeleka Yanga nje ya nchi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya
Awali ulikuwepo mpango wa mabingwa hao wa kihistoria kwenda kujichimbia katika moja ya nchi barani Ulaya kujiandaa na msimu mpya
Lakini mabadiliko ya ratiba kutokana na changamoto ya ugonjwa wa corona yamepelekea mpango huo kufutwa
Aidha tayari TFF imetangaza kuwa msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom utaanza Setpemba 06 ikiwa Yanga imeanza mazoezi bila ya nyota wake wa kigeni wanaotarajiwa kuanza kuwasili kesho Jumamosi
"Hatutaweza kwenda kuweka kambi nje ya nchi kutokana na muda kuwa mdogo. Tayari TFF imetangaza ligi itaanza Septemba 06, timu imeanza mazoezi lakini bado baadhi ya wachezaji hawajafika kutokana na changamoto ya usafiri. Ndani ya muda mfupi pia tutakuwa na Tamasha la wiki ya Mwananchi," alisema Injinia Hersi
Yanga tayari imeanza maandalizi chini ya kocha msaidizi Riedoh Berdien