Kwa Lwandamina pointi tatu ndio muhimu zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Nov 2017
Kwa Lwandamina pointi tatu ndio muhimu zaidi
Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema, anachoangalia ni ushindi na pointi tatu tu, na kuhusu mabao mengi ni kwa ajili ya kuwaongezea wachezaji wake hali ya kujiamini.

Lwandamina amesema, anachoangalia ndani ya kikosi chake ni ushindi wa pointi tatu na siyo idadi ya mabao kwa sababu ushindi wa namna hiyo ni kwa ajili ya kuongeza hali ya kujiamini.

"Katika mchezo unachokiangalia ni pointi tatu tu, ukishinda bao moja na matano pointi ni zile zile, lakini uzuri wa kuwa na idadi kubwa inasaidia kuwajenga wachezaji kuwa na hali ya kujiamini,"alisema Lwandamina.

"Hata hivyo ni kawaida kwa kocha kufurahia timu inapofanya vizuri, tunashukuru na lengo ni kuona tunafanya vizuri kila mchezo na kusonga mbele zaidi."

Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi na pointi 20 nyuma ya Simba inayoongoza na pointi 22 ambazo ni sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’