Huyu Farid lazima awalaze watu na viatu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Aug 2020
Huyu Farid lazima awalaze watu na viatu

Jana klabu ya Yanga ilitangaza kumsajili winga wa kimataifa wa Tanzania Farid Mussa kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Winga huyo aliyekuwa akikipiga katika klabu ya soka ya Tenerife ya Hispania amemaliza mkataba wake huko na kujiunga na mabingwa wa kihistoria kama mchezaji huru.

Akizungumzia usajili wa mchezaji huyo jana Msemaji wa Yanga Hassan Bumbuli alisema umetokana na mahitaji, walikuwa wakihitaji winga mwenye kasi na uwezo mzuri.

"Tunaamini Farid ni chaguo sahihi kwa sasa ndani ya timu ya wananchi na tunafurahi kukamilisha usajili wake,"alisema

Kabla ya kwenda Hispania kucheza soka la kulipwa aliitumikia Azam FC kwa misimu mitatu 2013 hadi 2016 akitokea kwenye kituo cha kulea vipaji cha klabu hiyo na baadaye akajiunga na Tenerife kwa majaribio na kufuzu.

Meneja wa mchezaji huyo Jemedari Said amesema kuwa kabla ya kusaini kulikuwa na majadiliano marefu baina ya mchezaji na Yanga kwa zaidi ya siku 10 ili kurekebisha mkataba huo.

Kwa mujibu wa Jemedari, Farid bado ana ndoto ya kwenda mbali zaidi hivyo, alitaka moja ya kipengele ni kuruhusiwa kuondoka iwapo atapata timu nje ya nchi.

Huyo ni mchezaji wa nane kusajiliwa Yanga mpaka sasa. Wengine ni Shomari Kibwana, Yassin Mustapha, Bakari Mwamnyeto, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Zawadi Mauya, Waziri Junior na Yacouba Songne.

Yanga bado inaendelea na usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.

Uongozi wa klabu hiyo ulipania kufanya marekebisho ya kikosi hicho ili kurudi katika kasi kupigania taji la ligi baada ya kukosa kwa misimu mitatu mfululizo.

Ujio wa Farid umepokewa kwa shangwe na mashabiki wa Yanga, wengi wakiwa na matumaini kuwa atairejesha Yanga katika hadhi yake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’