Misimu miwili iliyopita haikuwa mizuri kwa winga Juma Mahadhi ambaye alikuwa nje ya uwanja tangu August 2018 baada ya kupata majeraha makubwa ya goti
Mahadhi aliutumikia kwa kiasi kidogo mkataba wake mpya aliokuwa amesaini na Yanga
Ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa na bila shaka ndio maana uongozi wa Yanga umempa nafasi nyingine kwa kumpa mkataba mpya
Kwa sasa Mahadhi yuko fiti, ana jukumu la kuhakikisha anawadhihirishia Wanayanga thamani yake
Tangu kuondoka kwa kina Simon Msuva, ni Mahadhi aliyekuwa akionekana kama mchezaji anayeweza kuziba pengo la Msuva kabla ya kupata majeraha yaliyomuweka nje muda mrefu
Hii ni nafasi adimu kwake, Wanayanga wanasubiri kuona nini ataifanyia Yanga msimu huu
Baada ya kukaa nje kwa muda mrefu, atakuwa kama ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga
Hivyo atapaswa kuwania nafasi kwa kumshawishi kocha wa Yanga ambaye bado uongozi haujamuweka hadharani