Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemtangaza winga Bernard Morrison kuwa mchezaji huru baada ya kubaini mapungufu katika mkataba wake wa miaka miwili aliosaini Yanga
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Elias Mwanjala amesema mkataba wa Yanga na Morrison, una mapungufu makubwa
Hivyo shauri hilo lililochukua siku mbili limetamatishwa hivyo
Aidha kwa fedha ambazo Mghana huyo alichukua klabu ya Yanga ametakiwa kuzirudisha na wakati huohuo amepelekwa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kutokana na tukio la baada ya kusaini mkataba na Simba tarehe 8/8 wakati ana kesi yake ya kimkataba kwenye kamati
ADVERTISE HERE