Sureboy awaomba Azam Fc wamruhusu atue Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Aug 2020
Sureboy awaomba Azam Fc wamruhusu atue Yanga

Uongozi wa klabu ya Azam Fc unatajwa kuwa kikwazo kwa nyota Salum Abubakar 'Sureboy' kujiunga na klabu ya Yanga

Taarifa zilizopatikana mapema leo, zimebainisha kuwa Sureboy amewaandikia barua viongozi wa Azam Fc akiwaomba wasikilize ofa iliyotolewa na Yanga ili aweze kujiunga na timu hiyo

Yanga imeshapeleka ofa mbili kwa Azam Fc wakitaka kumsajili kiungo huyo fundi aliyebakisha mwaka mmoja na wauza ice-cream hao

Inaelezwa ofa ya kwanza ya Tsh Milioni 20 ilikataliwa , Wakapeleka ofa nyingine ya Tsh Milioni 35 ikakataliwa pia, wao Azam wakitaka Tsh Milioni 70 waweze kumuachia kiungo huyo

Jana uongozi wa Azam Fc ulitangaza kumuondoa sokoni Sureboy wakimjumuisha kwenye kikosi chao kinachojiandaa na ligi kuu inayoanza Septemba 06

Ni wazi hata wakimlazimisha, Sureboy hatacheza kwa furaha kwani tayari mawazo yake yapo Yanga

Ni vyema Azam Fc na Yanga wakakutana mezani kujadiliana kwa kina ili kuweza kufanikisha ndoto ya Sureboy kuweza kuichezea Yanga

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’