Mshamuliaji wa Yanga Amissi Tambwe amewamwagia sifa Obrey Chirwa na Emanuel Martin ambao jana waliisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mbeya City.
Mkali huyo wa mabao amesema sasa kazi ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne imeanza rasmi.
Aidha amesema anashukuru amepona majeraha yake ya goti yaliyomuweka nje mpaka sasa na anasubiri kwa hamu kurejea dimbani.
Tambwe tayari ameanza mazoezi mepesi na anatarajiwa kuwa fiti kabisa na kurejea dimbani pengine baada ya mapumziko ya michuano ya Chalenji inayoanza Disemba 03 hadi Disemba 17.
"Nafarijika kuona kidogo nimeanza kuwa fiti japo nimekatazwa kufanya mazoezi ya nguvu hadi niimarike zaidi vinginevyo mambo yatakuwa ndivyo sivyo," amefunguka Tambwe.
Tambwe amesisistiza kuwa haofii mechi zilizokwishachezwa kwenye Ligi Kuu hadi sasa, mpango wake ni kuchukua kiatu cha dhahabu mwishoni mwa msimu bado uko palepale.
"Ligi bado sana, najua nitakosa mechi kama 12 hadi 14 za mzunguko wa kwanza, lakini nitakapokuwa fiti na kuanza kucheza lazima nitimize ndoto yangu ya kuwa mfungaji bora," alisema.

ADVERTISE HERE