Mshambuliaji Yacouba Sogne raia wa Ivory Coast amethibitisha kuwa tayari amemwaga wino kuwatumikia mabingwa kihistoria Yanga, akitarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni
Sogne amethibitisha ujio wake Yanga kupitia video fupi iliyowekwa hadharani Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said
Yacouba amewatoa hofu mashabiki wa Yanga kuwa wamsubiri, kwani atawasili nchini hivi karibuni
Sogne anatarajiwa kuwa mshambuliaji kiongozi katika safu mpya inayosukwa na uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na GSM
Hata hivyo, inaelezwa bado kuna mshambuliaji mwingine wa kigeni anasubiriwa
Je ni Heritier Makambo aka Makambovic? tusubiri...!
Kwa hakika yajayo yanafurahisha, msimu ujao wataokota sana mipira nyavuni..!
ADVERTISE HERE