Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars leo inashuka dimbani huko kusini mwa Afrika kuumana na wenyeji wao Afrika Kusini katika mchezo wa robo fainali kombe la Cosafa.
Stars iliyoalikwa kwenye michuano hiyo, ilitinga robo fainali baada ya kuibuka kidedea wa kundi A kwa kujikusanyia jumla ya alama tano sawa na Angola, Stars ikifuzu kwa idadi ya mabao.

Stars inayotumia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi ya CHAN, inahitaji kushinda na kutinga nusu fainali kuzifuata Zambia na Lesotho zilizofuzu jana.
Hautakuwa mchezo mwepesi kwa kuwa Stars itapambana na wenyeji wa michuano hiyo.
Afrika Kusini imekuwa na kawaida ya kutumia michuano hii kuwapa nafasi wachezaji wa kikosi cha vijana.
Likifanyika hilo Stars itakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi kwani kikosi cha kocha Mayanga kiko imara sana,
Kuletewa kikosi cha vijana itakuwa kurahisishiwa kazi.

ADVERTISE HERE