Awamu ya kwanza ya mchakato wa Mabadiliko mfumo wa uendeshaji klabu ya Yanga itakamilika August 30 2020
Uongozi wa Yanga tayari umeweka wazi kuwa baada ya tarehe hiyo, kutaitishwa Mkutano Mkuu wa Wanachama kwa ajili ya kupitisha mfumo uliopendekezwa
Wakati hayo yakisubiriwa, pale Makao Makuu, ujenzi wa duka kubwa la kuuza vifaa michezo klabu ya Yanga utafanyika
Ujenzi huo ukikamilika, utaifanya Yanga iwe klabu ya kwanza kumiliki duka hilo la kisasa ambalo litakuwa chanzo kikubwa cha mapato ya klabu
Kwa miaka mingi mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku kuona miradi ya aina hiyo inaanzishwa ili kuiwezesha timu kuwa na vyanzo vingi vya mapato
Hakuna shaka, huko tuendako ni kuzuri zaidi, dalili njema zinaonekana




ADVERTISE HERE