Achana na mjadala kuhusu klabu ya Yanga kutoingiza mchezaji hata mmoja kwenye kikosi bora cha msimu ligi kuu ya Vodacom katika tuzo zilizotolewa jana pale Mlimani City
Mjadala mkali umeibuka wadau wakihoji vigezo vilivyotumika kumjumuisha mshambuliaji wa Simba John Bocco kwenye kikosi hicho licha ya kuwa wapo washambuliaji wengine waliofanya vizuri zaidi yake
Hebu angalia takwimu za washambuliaji hawa na jiulize ilikuwaje nahodha huyo wa Simba akawazidi vigezo?
Yusufu Muhilu - Magoli 13 assist 3
Peter Mapunda - Magolli 13 assist 5
Obrey Chirwa - Magoli 12 assist 1
Reliants Lusajo - Magoli 12 assist 4
Waziri Junior - Magoli 13 assist 2
Bocco alimaliza msimu akiwa amefunga mabao nane na kutoa pasi mbili za mabao
Ni wazi kama kigezo ilikuwa kuisaidia timu basi washambuliaji hao hapo juu walistahili kuwa na kipaumbele juu ya Bocco
Mapunda wa Mbeya City alihusika kwenye mabao 18 ya timu yake, wakati Mhilu na Lusajo walihusika kwenye mabao 16, Waziri Jr akahusika kwenye mabao 15, Chirwa kahusika katika mabao 13 na Bocco amehusika kwenye mabao 10 tu
Kwa hakika soka letu lina mambo mengi ya kushangaza..!