Wakimtangaza watadhihirisha ni wao waliompa kiburi - Injinia Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2020
Wakimtangaza watadhihirisha ni wao waliompa kiburi - Injinia Hersi

Mkurugenzi wa uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema kama klabu ya Simba itatangaza kumsajili mshambuliaji Bernard Morrison leo, basi watadhihirisha kuwa ni wao waliokuwa wakimpa kiburi na kumfanya awe mtovu wa nidhamu ndani ya Yanga

Tetesi za klabu ya Simba kuwa mbioni kutangaza kumsajili Mghana huyo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwaacha mashabiki wa Yanga wakishikwa na mshangao

Akihojiwa na redio moja maarufu kuhusu tetesi hizo, Injinia Hersi alisema anachofahamu suala la Morrison bado halijapatiwa ufumbuzi na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji hivyo kama Simba itatangaza kuwa imemsajili kabla ya mamauzi ya Kamati ni wazi watadhihirisha kuwa ni wao waliokuwa wakimfanya mchezaji huyo awe na kiburi

"Kitakuwa kitu cha ajabu sana, ikiwa watamtangaza leo basi wataudhihirishia umma kuwa wao ndio waliokuwa wanahusika kumpa kiburi kwa yale aliyekuwa anayafanya nje na ndani ya uwanja"

"Kwani ifahamike bado kuna kesi kwenye kamati ya sheria na hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)," alisema

Kamati hiyo inatarajiwa kuweka hadharani hukumu ya sakata hilo Jumatatu, August 10 2020

Morrison alisajiliwa na Yanga mwezi Januari kwa mkataba wa miezi sita

Hata hivyo kulingana na taarifa iliyotolewa mapema na Yanga, baada ya kuridhishwa na uwezo wake, Mghana huo alipewa mkataba wa miaka miwili ambao aliusaini March 20 2020

GSM kupitia Injinia Hersi ndio waliofanya mzungumzo nae na makubaliano kufikiwa kabla ya nyota huyo kusaini mbele ya Mwanasheria wa Yanga Simon Patrick ambaye kwa sasa ni Kaimu Katibu Mkuu

Hata hivyo Morrison amekana kusaini mkataba huo akidai kuwa saini yake imeghushiwa. Madai hayo yalipelekwa kwa Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi

Kuweka msisitizo kuwa Morrison ni mchezaji wao halali, Yanga imemjumuisha kwenye kikosi chake kuelekea msimu ujao wa ligi kuu ya Vodacom ambao utaanza Septemba 06 2020

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’