Safu ya ulinzi ya Yanga imekamilika baada ya usajili wa beki kisiki Abdallah Shaibu Ninja
Ninja anaungana na Bakari Nondo Mwamnyeto, Said Juma Makapu na Lamine Moro
Yanga ni kama imemaliza mahesabu katika eneo la safu ya ulinzi wa kati baada ya usajili wa Ninja
Eneo hilo sasa linaundwa na watu wa kazi kwelikweli
Ni matumaini ya kila mmoja kuwa yale makosa yaliyojitokeza msimu uliomalizika katika eneo hilo yatapungua kwa kiasi kikubwa

Kocha wa Yanga atakuwa na mtihani wa kutengeneza pacha ya walinzi hao wa kati
Lamine na Makapu ndio waliokuwa chaguo la kwanza wakati wa kocha Luc Eyamel lakini mambo yanaweza kubadilika baada ya ujio wa Mwamnyeto na Ninja
Ukimuondoa Ninja, mabeki wengine Lamine, Makapu na Mwamnyeto walikuwa wakicheza kwenye vikosi vya kwanza vya timu zao

Makapu sasa ameiva katika eneo la ulinzi na bila shaka atawapa changamoto Lamine na Mwamnyeto katika kikosi cha kwanza
Licha ya kutokuwepo hapa nchini, kama Ninja atakuwa na ubora alioondoka nao msimu uliopita, ni wazi nae ataongeza ushindani wa namba

Kwa muda aliokaa Marekani, ni wazi Ninja atakuwa amenufaika, kwani alikuwa akifanya mazoezi katika taasisi yenye walimu na vifaa bora
Ligi ya hapa Bongo haiwezi kuwa changamoto kwake