Baada ya mwafaka kushindwa kufikiwa na wakongwe Kelvin Yondani na Juma Abdul, inaelezwa Yanga imeanza kupiga hesabu kusaka mbadala wa wachezaji hao nafasi ya beki wa kulia ikipewa kipaumbele zaidi
Jana kupitia mahojiano yake na chombo kimoja cha habari, Abdul ni kama aliwaaga mashabiki kuwa anaangalia kwingine baada ya kutokubaliana na ofa aliyopewa na Yanga
Yanga inaweza kumrejesha mlinzi wake wa zamani Hassan Ramadhani 'Kessy' aliyemaliza mkataba kunako klabu ya Nkana Fc ya nchini Zambia
Majuzi Kessy alionekana kwenye viunga vya Makao Makuu ya klabu ya Yanga ikielezwa kuwa kwenye mazungumzo na mabosi wake hao wa zamani
Pamoja nae, mlinzi wa kulia wa Mtibwa Sugar Kibwana Shomari nae amekuwa akitajwa kuwaniwa na mabingwa hao wa kihistoria
ADVERTISE HERE