Sababu ya maproo kuchelewa yatajwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Aug 2020
Sababu ya maproo kuchelewa yatajwa

Baada ya utambulisho wa usajili wa wachezaji wanne wa ndani, mashabiki wa Yanga wamekuwa na shauku ya kutaka kuwafahamu nyota wa kigeni waliosajiliwa na timu hiyo

Hata hivyo huenda watalazimika kusubiri mpaka wiki ijayo kutokana na changamoto ya usafiri wa anga katika baadhi ya nchi ambazo wachezaji hao wanatoka

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amewahakikishia Wanajangwani kuwa wameshakamilisha usajili wa nyota wote wa kigeni lakini sababu ya kutowasili mpaka sasa ni kutokana na changamoto hiyo ya usafiri wa anga

"Tumesha malizana na wachezaji wa nje, changamoto iliyopo ni anga kufungwa kwa baadhi ya nchi ambazo wachezaji wetu wanatoka. Tunatarajia kuanzia tarehe 15 wataanza kuingia nchini, kwa sasa tutaendelea kutambulisha wachezaji wa ndani ya nchi," alisema Injinia Hersi ambaye ndiye msimamizi mkuu wa michakato ya usajili kwa upande wa GSM ambao wanahusika na gharama za usajili msimu huu

Yanga inatarajiwa kuanza mazoezi siku ya Jumatatu, wakitarajia kuanza na wachezaji wa ndani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
1h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’