Baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga, mshambuliaji Waziri Junior amewaahidi mashabiki kuwa watarajie furaha kurejea kwani amejipanga kuendeleza moto wa kuzifumainia nyavu aliomalizanao Mbao Fc
Msimu uliomalizika Junior aliifungia Mbao Fc mabao 13 kwenye ligi huku akiongeza mabao mawili kwenye mchezo wa play-off dhidi ya Ihefu Fc ambao uliishuhudia Mbao ikishuka daraja licha ya ushindi wa mabao 4-2 baada ya kupoteza 2-0 kwenye mchezo wa ugenini
"Nimefurahi kujiunga na Yanga, ni timu nyingi zilizokuwa zikinihitaji lakini ni Yanga waliokuja na ofa nzuri. Mimi kazi yangu ni kufunga mabao, hivyo nimejipanga kuhakikisha natimiza majukumu yangu na kuwapa furaha mashabiki wa Yanga," alisema Junior
Yanga inasuka upya safu yake ya ushambuliaji baada ya kumaliza msimu ikiwa imefunga mabao machache
Tayari mabingwa hao wa kihistoria wametangaza kuachana na washambuliaji David Molinga, Yikpe Gnamien na Tariq Seif Kiakala
Junior amesajiliwa kuchukua nafasi ya Kiakala wakati washambuliaji wawili wa kigeni wanatarajiwa kutua kuchukua nafasi za Molinga na Yikpe