Baada ya hapo jana Afisa Habari wa Azam Fc Thabit Zacharia 'Zakazakazi' kupitia mahojiano na chombo kimoja cha habari kutamka kuwa hawamuuzi kiungo Salum Abubakar pamoja na kupokea ofa ya Yanga, inaelezwa Sureboy ameomba kuondoka kunako waoka mikate hao
Yanga imeonyesha nia ya kumtaka Sureboy, ikiwa tayari kuvunja mkataba wake wa mwaka mmoja ili ajiunge na mabingwa hao wa kihistoria
Habari zilizopatikana mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Azam Fc Abdulkarim Amin 'Popat' amethibitisha kuwa Sureboy ameomba aachwe akatafute changamoto mahali pengine
"Yanga walileta ofa rasmi katika klabu ya Azam FC yakumtaka kiungo Salum Abubakary (Sure Boy) na mchezaji mwenyewe ameiomba klabu aondoke akapate changamoto mpya," alisema Popat
Yanga inatarajiwa kuwasilisha ofa nyingine ambayo itazikutanisha mezani timu hizo kujadili mustakabali wake
Sureboy ameitumikia Azam Fc kwa miaka 10, huu ni wakati wake sahihi kupata changamoto mahali pengine