Hatma ya Morrison August 10

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Aug 2020
Hatma ya Morrison August 10

Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Elias Mwanjala, amesema uchunguzi wa kesi ya winga Bernard Morrison dhidi ya klabu ya Yanga umekamilika na maamuzi yake yatawekwa hadharani August 10 2020

Mwanjala amesema suala la Morrison na Yanga limechukua muda mrefu wakisubiri kukamilika kwa uchunguzi

Aidha, Mwanjala amesema kwa kuwa suala hilo lilikuwa likihusisha masuala yaliyohitaji uchunguzi wa kipolisi, waliliachia Jeshi la Polisi lifanye kazi yake

Morrison aliukana mkataba mpya wa Yanga akidai saini iliyo kwenye mkataba huo imeghushiwa

Yanga ilitangaza kumuongezea Morrison mkataba mpya wa miaka miwili mwezi March baada ya kuridhishwa na kiwango chake

Lakini pia Yanga iliwasilisha malalamiko TFF ikiituhumu klabu ya Simba kuingilia mkataba wa nyota huyo kinyume na utaratibu

Mwanjala amesema maamuzi ya kesi zote yatatolewa August 10 sambamba na kesi nyingine mbalimbali zilizowasilishwa mapema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
22h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’