Aliyekuwa nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi ameeleza kushitushwa na kutemwa kwenye kikosi cha timu hiyo kuelekea msimu ujao
Mcongomani huyo amesema kuwa ni jambo ambalo hakuwa akilitarajia lakini amekubaliana na uamuzi huo hivyo anajipanga kurejea kwao DR Congo
"Si umesikia mwenyewe wametangaza? wametangaza hakuna ubaya, wao wametaja wachezaji walioachwa na mimi nimo, sina namna ila dah. . acha tu.."
"Muda wowote ntaondoka ntarudi Congo nikafikirie hatma yangu, lazima niende nyumbani bado sijajua naelekea wapi"
"Ni taarifa ambazo sikutegemea ila uongozi ndo wanajua siwezi kuongelea sana, ila waache kumpakaza mtu maneno aonekane mbaya, bwana eeh ni story ndefu nikianza kukuelewesha ila kila mtu abaki na ukweli wake kama siku imefika basi imefika ila nawatakia kila la heri dah...," alisema Tshishimbi
Tshishimbi ni kama alijiharibia mwenyewe kwani uongozi wa Yanga ulimpa mkataba mpya tangu mwezi March mwaka huu lakini baadae akageuka makubaliano ya awali akitaka aongezewe pesa kwa kisingizio kuwa klabu ya Simba imeahidi kumpa ofa nono zaidi
Uongozi wa Yanga ulimpa wiki mbili kuamua kusaini mkataba au la, lakini Mcongoman huyo akaendelea kuvutana na mabosi wake kupitia vyombo vya habari
Baada ya Yanga kumsajili Zawadi Mauya kutoka Kagera Sugar, ndio ukawa mwisho wa Tshishimbi kwenye kikosi cha Yanga