Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza kufanya mabadiliko katika benchi lake la ufundi wakiwabakisha Redoh Braden, kocha msaidizi na Fareed Cassim mtaalamu wa misuli
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga mapema leo, imebainisha kuwa makocha hao wataungana na kocha mkuu anayesubiri kutangazwa
Aidha, aliyekuwa kocha msaidizi Charles Mkwasa amemaliza mda wake wakati kocha wa makipa Peter Manyika, Meneja wa timu Abeid Mziba na Mtunza vifaa Fred Mbuna hawa wamebadilishiwa majukumu
Taarifa hiyo imebainisha kuwa watakaoziba nafasi zao watatangazwa baadae
ADVERTISE HERE