Tetesi zimeongezeka viunga vya Jangwani baada ya hapo jana mabingwa hao wa kihistoria kutangaza kuacha wachezaji 14 kwa mpigo
Ni uamuzi mgumu sana uliochukuliwa kuacha idadi hiyo ya wachezaji, lakini mabosi wakawatoa wasiwasi mashabiki wa Yanga kuwa wataziba nafasi zote
Achana na tetesi za Sure Boy, mwamba huyu Farid Mussa aliyekuwa akikipiga klabu ya Tennerife Fc inayoshiriki ligi daraja la pili kule Hispania, anarejea nchini
Za chinichini ni kuwa anaweza kuwa miongoni mwa watakaovaa uzi wa njano na kijani msimu ujao
Farid ni mchezaji mwenye uzoefu, kazi yake anapokuwa kwenye timu ya Taifa inathibitisha ubora wake, pengine sio wakati tu kwake kupata timu kubwa
Lakini ndani ya Yanga ambayo iko kwenye ushirikiano na La Liga na Sevilla, anaweza kupata nafasi nyingine ya kuonekana kwani moja ya sehemu ambazo Sevilla na Yanga zitashirikiana ni katika maboresho ya benchi la ufundi pamoja na wachezaji
Mchezaji anaweza kutoka Yanga moja kwa moja na kutua timu ya vijana ya Sevilla na hata ile ya wakubwa kama atakidhi vigezo
Lakini pia Sevilla inaweza kutoa wachezaji wakajiunga na Yanga iwe kwa mkopo au kwa makubaliano maalum
Wapo watakaombeza kama atarejea nchini kutoka Ulaya, lakini ni mchezaji mwenyewe anayefahamu lile analofanya
Pia wakati mwingine kuanza upya ni njia ya kujipanga kwa ajili ya mafanikio makubwa zaidi