Ukizungumzia viungo bora kwenye ardhi ya Tanzania katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, huwezi kukosa kutaja jina la Salum Abubakar 'Sureboy' anayekipiga kunako klabu ya Azam Fc
Ni mchezaji aliyedumu kwenye kiwango cha juu kwa muda mrefu, si ajabu kuona karibu katika kila dirisha la usajili, Sureboy amekuwa akihusishwa na Yanga
Kuna wakati mashabiki wa Azam walimtuhumu kuwa na mapenzi na Yanga, na kuwa huwa anacheza chini ya kiwango anapokutana na Yanga, tuhuhuma hizi alizikanusha
Kwa sasa jina lake linatajwa sana huko mitandao akitajwa kuwa amamelizana na mabingwa hao wa kihistoria
Huyu ni mchezani ambaye kama kweli mabosi wa Yanga wamemnasa, basi msimu ujao kuna watu waandike maumivu kwani huo mziki wa Yanga eneo la kiungo hautazuilika
Huu ni usajili ambao Wanayanga wameusubiri kwa misimu kadhaa, bila shaka GSM watatimiza ndoto ya kumnasa fundi huyu mtoto wa Mwanayanga, mkongwe Abubakar Salum 'Sureboy' orijino!
Β