Mrisho Ngassa hajawahi kuficha mapenzi yake kwa Yanga. Ni mmoja wa wachezaji waliopata mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha Yanga.
Wakati ule akiwa Yanga Ngassa aliifanya kazi yake kwa ustadi na mapenzi yasiyo na shaka.
Ilikuwa bahati mbaya kwake toka aondoke Yanga ameshindwa kufikia kile kiwango chake cha wakati ule ingawa sasa anaonekana kuimarika zaidi.
Msimu huu Ngassa amekuwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa kikosi cha Mbeya City. Leo anatarajiwa kuwaongoza vijana hao kutoka jiji la Mbeya kuikabili timu anayoipenda sana, Yanga.
Hakuna shaka kuwa winga huyo machachari ni lazima achungwe sana na safu ya ulinzi ya Yanga. Licha ya mengi yanayosemwa juu yake, Ngassa bado anao uwezo ya kufanya yale yasiyotarajiwa na wengi.
Ikumbukwe Ngassa alikuwa miongoni mwa waliopendekezwa kusajiliwa wakati wa dirisha kubwa la usajili kuchukua nafasi ya Simon Msuva.
Jaribio lake la kurejea Jangwani lilikwama kwenye dakika za majeruhi.
Sasa Ngassa atataka atumie nafasi hii kuwakosoa wale waliomkataa kurejea wakati ule.
Lakini pia kwa kuwa dirisha dogo la usajili limefunguliwa na bado Yanga inaonekana kushindwa kutibu ugonjwa ulioachwa na Simon Msuva, atataka kuwapa nafasi nyingine ya kufikiria upya wale waliomkataa mwanzo.
Ngassa anafaa kuchungwa zaidi katika mchezo wa leo kama atapata nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha kwanza cha Mbeya City.

ADVERTISE HERE