Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mrisho Ngasa amewaaga mashabiki wa timu hiyo baada ya kupewa mkono wa kwaheri
Baada ya kikao kilichofanyika leo baina ya wachezaji na viongozi wa Yanga, Ngasa amethibitisha kuwa ni mmoja wa wachezaji waliotemwa
"Kwanza nitoe shuklani zangu kwa wote tuliokuwa pamoja ktk kipindi chote Yanga viongozi wangu mashabiki na wachezaji wenzangu"
"Kwa kikao kilichofanywa leo sitakuwa katika kikosi cha yanga niwatakie mafanikio yalio mema Enjoy soccer", aliandika Ngasa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Jana uongozi wa Yanga uliwataka mashabiki kukubaliana na maamuzi yaliyofikiwa kuwaacha baadhi ya wachezaji licha ya kuwa wanaweza kuwa wanawapenda sana
Ni katika jitihada za kusuka upya kikosi chenye ushindani
ADVERTISE HERE