Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amepania kuiona timu yake ikibeba taji la nne kwa kuzichukua pointi tatu za Mbeya City ambayo watacheza nayo leo Novemba 19.
Huo ni mchezo wa mzunguko wa 10, kwa timu zote mbili huku Yanga wakiwa kwenye nafasi ya tatu kwenye msimamo kwa kujikusanyia pointi 17, wakati Mbeya City wapo katika nafasi ya nane wakiwa na pointi 11.
Timu zote mbili zitaingia uwanjani zikiwa na matokeo tofauti katika mechi zao za mwisho Mbeya City walikuwa nyumbani uwanja wa Sokoine wakapoteza kwa bao 1-0, dhidi ya Simba wakati Yanga walikuwa ugenini uwanja wa Namfua Singida na kutoka suluhu ya bila kufungana.
Matokeo haya yanaufanya mchezo kuwa mgumu na wenye ushindani mkubwa kwani wenyeji Yanga watataka kushinda ili kuzuidi kuifukuzia nafasi ya kwanza ambayo inashikiliwa na mahasimu wao Simba.
Kocha George Lwandamina, amekuwa na timu kwa siku nne kwenye mazoezi tangu aliporudi nchini akitokea kwao Zambia alipokwenda kuhudhuria msiba na amejivunia kiwango cha wachezaji wake na kurejea kwa mshambuliaji Amissi Tambwe aliyeanza kufanya mazoezi mepesi na timu wiki hii.
Mzambia huyo ataendelea kuwategemea Obrey Chirwa na Ibrahim Ajibu katika umaliziaji baada ya Donald Ngoma, kuendelea kuwa nje kutokana na majeruhi ya goti ambayo yanamkabili kwa muda sasa sambamba na kiungo Thabani Kamusoko.
Endapo Yanga itashinda itafikisha pointi 20 ambazo zitazidi kuweka hai matumaini yao ya kutetea ubingwa wao kwa mara ya nne, jambo ambalo siyo rahisi sana msimu huu.
Kwaupande wake kocha msaidizi wa Mbeya City Mohamed Kijuso, amesema huo kwao ni mchezo mgumu lakini watajipanga kuhakikisha wanacheza vizuri na kupata ushindi bila kujali wanacheza na timu gani na uwanja gani.
Mrisho Ngasa ni mmoja wa washambuliaji ambao watakuwepo kwenye kikosi cha City na anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya timu yake sambamba na mshambuliaji Mohamed Mkopi ambaye msimu huu ameshindwa kuonyesha makali yake hadi sasa.
Kazi kubwa ambayo itawakabili City ni kuwazuia washambuliaji wa Yanga Chirwa na Ajibu ambao msimu huu, wameonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali na wanahitaji ulinzi wa ziada ili kuzuiliwa.
Ally Babu, Haruna Shamte ni miongoni mwa wachezaji ambao wanatarajiwa kufanya kazi kubwa na kuwazuia nyota hao wasiweze kupata matokeo licha ya kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Uhuru.

ADVERTISE HERE