Utambulisho kuhamia 'anga' za Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 Aug 2020
Utambulisho kuhamia 'anga' za Kimataifa

Baada ya kutambulishwa usajili wa nyota kadhaa wa ndani, Yanga inatarajiwa kuanza kutambulisha usajili wa nyota wake wa kigeni

Mpaka sasa Yanga imekamilisha usajili wa wachezaji wanne wa ndani ambao ni mlinzi wa kushoto Yassin Mustafa kutoka klabu ya Polisi Tanzania, mlinzi wa kati Bakari Nondo Mwamnyeto kutoka klabu ya Coastal Union

Wengine ni kiungo mkabaji Zawadi Mauya kutoka klabu ya Kagera Sugar na mshambuliaji Waziri Junior aliyetua jana akitokea klabu ya Mbao Fc ambako alimaliza msimu kwa kupachika jumla ya mabao 15 kwenye ligi na mechi za play-off

Jana baada ya kutangaza usajili wa Junior, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick alisema sasa wanahamia upande wa nyota wa kigeni

Kumekuwa na tetesi nyingi kuwahusu baadhi ya wachezaji ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakitajwa kumalizana na Yanga

Ukweli wa tetesi hizo utafahamika kuanzia leo Jumatatu

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wamefanya kile walichoahidi akiwataka mashabiki wakae tayari kuwapokea wachezaji hao

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’