Unamfahamu yule beki kisiki wa Liverpool Virgil Van Dijk? Basi Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amewafananisha beki huyo pamoja na beki mpya wa Yanga Bakari Nondo Mwamnyeto kuwa umahiri wao ni kama zilivyo sifa za mlima Kilimanjaro
Kupitia mtandao wake wa kijamii, Simon ameandika haya
"Katika pitapita za Airbus, imekutana na Mlima Kilimanjaro nikaona niwajuze kitu ambacho watu wengi pengine hawajui kuhusu mlima huu"
"Mlima Kilimanjaro ndio mlima mrefu zaidi kuliko yote duniani uliosimama peke yake bila safu, yaani kwa kizungu tunasema "Kilimanjaro is the highest free-standing mountain in the world".
"Kama unafananisha milima na wachezaji basi mlima huu unaweza kuufananisha na wachezaji wawili tu duniani ambao ni “Virgil van Dijk” na “Bakari Nondo Mwamnyeto”, nikiwa na maana kwamba duniani kuna mabeki wengi wazuri lakini kwa watu wenye jicho la mpira Van Dijk ni beki mwenye vitu ambavyo huwezi kuviona kwa macho kama hauna jicho la mpira, kwa hapa bongo hivo vitu anavyo Mwamnyeto tu"
"Hivyo Mwenyezi Mungu aliamua kuumba milima mirefu sana duniani lakini akatupa watanzania kitu cha kipekee sana ambacho ni mlima Kilimanjaro, tujivunie kwa hilo"
"NB: Leo tupumzuke au tuendelee?"