Usajili wa Yanga unafanywa kisayansi sana kwani unazingatia kumaliza changamoto zilizojitokeza katika baadhi ya maeneo
Mapendekezo ya usajili wa mabingwa hao wa kihistoria yalishaandaliwa muda mrefu, Luc Eymael aliongezea tu lakini kazi kubwa ilishafanywa na Kamati ya ufundi Yanga
Tumeona kwenye nafasi ya ulinzi tayari mlinzi wa kati pamoja na mlinzi wa kushoto wameshatua, Bakari Nondo Mwamnyeto na Yassin Mustapha
Bado kuna mlinzi mwingine wa kushoto anasubiriwa na upande wa kulia, nako inaelezwa kuna jembe linasubiri kutambulishwa
Kiungo mkabaji tayari Zawadi Mauya ametambulishwa lakini inaelezwa yuko mwingine wa Kimataifa anasubiriwa. Huyo akitua maana yake Tshishimbi hana nafasi
Yupo mzawa mwingine kwenye nafasi ya kiungo cha uchezeshaji anatajwa kusubiri utambulisho! Huyu mara kwa mara amekuwa akihusishwa na Yanga, baba yake aliwahi kuwa winga matata sana kwenye kikosi cha Yanga miaka ya nyuma
Tusubiri kwani siku ya leo kuna jambo kubwa litatokea kama alivyosema Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz kuwa Jumapili hii haiwezi kupita hivi hivi
Baada ya hapo shughuli inahamia kwenye safu ya ushambuliaji, huko ndiko kila mmoja anasubiri kwa hamu...!