Kama kuna shabiki yeyote wa Yanga ana wasiwasi kuhusu maboresho ya kikosi yanayofanywa na uongozi chini ya usimamizi wa GSM, ondoa shaka kwani mambo mazuri yanakuja
Unachotakiwa kufanya ni kuandaa kiingilio chako kwa ajili ya siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi kwani siku hiyo itakuwa ni ufunguzi wa Yanga nyingine kabisa tofauti na ulizoziona ndani ya miaka mitatu iliyopita
Moja ya ahadi za Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ni kuunda kikosi imara kwa kushirikiana na uongozi wa Yanga ili kurejesha nyumbani ubingwa wa ligi kuu uliopotea kwa misimu mitatu
Nukuu ya kauli yake aliyoitoa mwezi uliopita : "Tutahakikisha mchezaji yeyote tunayemtaka tunampata. Hakuna mchezaji wa ndani ambaye tutashindwa kumsajili na wale wa nje angalau awe Grade B," alisema
Usajili wa beki Bakari Nondo Mwamnyeto ni ushahidi wa utekelezaji wa ahadi ambayo GSM waliwaahidi Wanayanga
Yanga imemsajili Mwanyeto kwa kununua mkataba wake kutoka Coastal Union, hakuwa mchezaji huru kama baadhi ya timu zinavyovizia mikataba ya wachezaji imalizike ndio wasajili
Ukiona nyota wa ndani hajasajiliwa na ulisikia sikia Yanga wanamtaka, basi fahamu hakuwa kwenye mipango huyo
Zawadi Mauya na Mwamnyeto, wamesajiliwa kwa kuwa walipendekezwa na utaona, hata Yanga kuna upungufu katika nafasi wanazocheza
Lakini shughuli ndio kwanza imeanza kwani GSM wanasema bado hawajaachia sapraizi, yaani ule usajili ambao kuna watu utawalaza mapema!