Tshishimbi alitikisa kiberiti Yanga, kakuta kimejaa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Aug 2020
Tshishimbi alitikisa kiberiti Yanga, kakuta kimejaa

Ukitaka kujua wapi pana vuja subiri mvua inyeshe. Bila shaka usajili wa Zawadi Mauya unaonesha wazi Yanga wameshagundua wapi panavuja.

Nadhani wote tunakumbuka Tshishimbi aliwaambia mashabiki wa Yanga done deal kupitia video aliyokuwa na Hersi Saidi

Hersi Saidi baadae akatolea ufafanuzi kuwa Papy alikubali kusaini hivyo wanasubiria aje asaini

Taarifa za ndani zinathibitisha kuwa Papy alikubali kusaini kwa mshahara wa Tsh 8m na dola 70,000 kama ada ya usajili kwa miaka miwili

Papy alipaswa kwenda kusaini siku ya 7/7 lakini hakutokea bila kutoa sababu jambo ambalo lilizua taharuki

Baadae akaenda kwa viongozi wa Yanga na kuwaambia kuwa kiasi kile ni kidogo hivyo wamuongezee hela

Wakaamuuliza kwanini akasema Simba wamempa ofa ya Tsh 12m kwa mwezi pamoja na ada kubwa ya usajili

Viongozi wa Yanga wakakerwa sana na kauli ya Papy kuwaambia kuwa amepewa ofa na Simba.

Yanga wamegundua kuna wachezaji wanatumia mgongo wa Simba kuwataka kutikisa viberiti.

Hivi unajua? :- Papy ndiye aliyeomba sana mechi dhidi ya Simba acheze licha ya kuwa alikuwa na injury

Akasema anataka gari aina ya Subaru ambayo inathaminiwa kuwa Tsh 18. Injinia Hersi akamwambia asaini atampa Milion 6.5 kutoka mfukoni mwake ili aongezee anunue hilo gari

Bado Tshishimbi alisimamia uamuzi wake akitaka gari, 18m za nyongeza na mshahara wa Tsh 12m kwa mwezi na Dola 70k kama ada ya usajili

Najiuliza, Papy nahodha imekuwaje amekuwa msaliti? Kwanini amekengeuka? Kwanini anatumia mgongo wa Simba?

Papy ana injury ambayo huenda ikamweka nje sio chini ya miezi 4. Mwisho wa siku tamaa itamponza na atakosa vyote.

Umri unakwenda, bado anataka mshahara mkubwa, bado ana injury, anachokitaka atakipata. Mheshimiwa Makamba alisema heshima na tamaa havikai nyumba moja.

Makala imeandikwa na Mwanahabari, Mchambuzi wa soka @privaldinho

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’