Mshambuliaji wa Yanga David Molinga amesema pamoja na changamoto alizokumbana msimu uliomalizia, anasikilizia dili la mkataba mpya
Akihojiwa na chombo kimoja cha habari jana, Molinga alisema zipo timu kadhaa zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili lakini anawapa kipaumbele waajiri wake wa sasa, Yanga
Molinga amesema kuwa anafurahia maisha ya kucheza soka hapa Tanzania, anawapenda mashabiki wa Yanga kwani wamekuwa chachu kwake kuongeza bidii pale asipofanya vizuri
"Nimebakiza mkataba wa mwezi mmoja na Yanga, ni kweli timu nyingi zinanihitaji nimepokea ofa lakini nawapa kipaumbele Yanga kwa sababu ni familia yangu na nimeizoea ligi naamini msimu ujao nitafanya vizuri," alisema Molinga
AKizungumzia changamoto alizokutana nazo msimu uliomalizika ikiwa ni pamoja na kuzomewa na mashabiki, Molinga alisema jambo hilo halimsumbui kwa sababu anafahamu mashabaki wanahitaji furaha wanapokwenda uwanjani hivyo unapokuwa hufanyi vizuri lazima utazomewa
"Mashabiki ndio wako hivyo ukifanya vibaya watakuzomea tu kwa sababu wao wanataka ufanye vizuri na hawakuzomei kwa ubaya Kwahio mimi naichukua kama chachu ya kunifanya nifanye vizuri"
Mcongomani huyo aliyedai kuwa na umri wa miaka 22 pia alitoa ufafanuzi wa lawama alizowahi kutoa kwa aliyekuwa kocha msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa kuwa hampendi
Amesema hana tatizo na kocha huyo na anamchukulia kama mzazi wake
"Hakuna shida yeyote kati yangu na Mkwasa, Yeye ni kama Baba yangu pale ninapokosea kama mwanaye lazima aoneshe kuwa hapa mwanangu sijapenda hivyo hakuna Utofauti wowote kati yetu"
Mkataba wake na Yanga unamalizika mwezi huu hivyo anasubiri hatma yake kama ataongezewa mkataba au la