Yanga leo imetangaza usajili wake wa kwanza wakimtambulisha kiungo mkabaji Zawadi Mauya aliyetua kutoka klabu ya Kagera Sugar
Mauya amemwaga wino wa miaka miwili, kukipiga na mabingwa hao wa kihistoria
Usajili wake unamuweka mtegoni nahodha Papy Tshishimbi ambaye anasuasua kusaini mkataba mpya
Tshishimbi amekuwa kwenye mvutano na Yanga tangu mwezi Machi akitaka aongezewe dau la usajili
Hata hivyo uongozi wa Yanga uliweka msimamo wakimtaka asaini mkataba kwa dau lilipo mezani, jana akipewa siku 14 kuamua
Inaelezwa Tshishimbi ameondoka leo kuelekea mapumziko DR Congo akiacha ujumbe kwa viongozi wa Yanga kuwa kama watamuhitaji atasaini mkataba mpya lakini kama itakuwa tofauti basi hatarejea nchini
ADVERTISE HERE