Mashabiki wa Yanga kwa wingi wao, wameonyesha shauku ya kutaka kufahamu ni wachezaji gani wamesajiliwa na mabingwa hao wa kihistoria
Lakini uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa wameshakamilisha usajili kwa asilimia 90 kinachosubiriwa ni kufunguliwa kwa dirisha la usajili kuanza kuweka hadharani majina ya wachezaji waliosajiliwa
Juzi Kaimu Katibu MKuu Simon Patrick aliwataka mashabiki wawe tayari na bando za kutosha kwenye simu zao kwani muda sio mrefu wataanza kuwafahamu wachezaji wapya
Dirisha la usajili litafunguliwa Jumamosi, August 01, 2020 ambapo kuanzia siku hiyo utaratibu wa kuwatambulisha wachezaji wapya utaanza
Imeelezwa, nyota wa kigeni waliosajiliwa wataanza kuwasili kuanzia siku hiyo
ADVERTISE HERE