Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Simon Patrick amesema kuwa nahodha wao Papy Tshishimbi walimpa muda aamue kama anabaki Yanga au aondoke
Patrick amethibitisha Tshishimbi kuwa na ofa ya Yanga mkononi na kuwa kama hatasaini ndani ya muda waliompa, basi wataachana nae
"Tumempa ofa yetu ya mkataba mpya mezani kama ataridhia tutaendelea nae na kama hataridhia tunajipanga kutafuta mbadala wake, " alisema
"Mkataba wake wa mwanzo utamalizika Agosti 12 na tulimpa wiki mbili afikirie kama ataendelea kubaki nasi au ataondoka. Kwa sasa hatutaki kuona mchezaji anakuwa juu ya klabu kama anataka kubaki asaini kwa mujibu wa mkataba tuliompa kama hataki basi aende hatuna muda wa kumbembeleza mtu"
Aidha, Patrick amesisitiza kuwa Yanga imetoa ofa kwa wachezaji wake kulingana na mahitaji ya timu na uwezo wa timu kwa sasa
Amesema kuwa wanajipanga kuwa na kikosi bora lakini chenye usawa kwa kiwango kikubwa