Nahodha wa Yanga Papy Tshishimbi atakuwa mchezaji huru kuanzia siku ya Ijumaa kama hatasaini mkataba mpya na mabingwa hao wa kihistoria, imefahamika
Pamoja na awali kutangazwa kuwa Mcongomani huyo alisaini mkataba wa miaka miwili, lakini imebainika kuwa hajarudisha mkataba wake aliosaini licha ya makubaliano na Yanga kufikiwa
Inaelezwa Tshishimbi ametaka aongezewe dau la usajili ndio amwage wino katika mkataba huo na kuendelea kubaki Jangwani
Amekuwa akihusishwa sana na klabu ya Azam Fc ingawa, msemaji wa Azam Thabit Zacharia amekana kutaka kumsajili Mcongomani huyo
Kama hatasaini mkataba mpya hadi kufikia siku ya Ijumaa, atakuwa mchezaji huru
ADVERTISE HERE