Kikosi bora cha Yanga msimu wa 2019/20

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2020
Kikosi bora cha Yanga msimu wa 2019/20

Baada ya msimu wa ligi kuu kumalizika huku Yanga ikiibuka katika nafasi ya pili, sio vibaya kuwaangazia wachezaji waliofanya vizuri zaidi kwa msimu mzima na kuwapa changamoto wengine kuhakikisha wanakuwa bora zaidi msimu ujao

1. Metacha Mnata

Pamoja na kusajiliwa kwa lengo la kuwa mlinda lango namba mbili mbele ya Mkenya Farouk Shikhalo, Metacha alipindua meza kibabe na kuwa chaguo la kwanza langoni

Alianza kuonyesha makali yake kwenye michuano ya ligi ya mabingwa kule Botswana ambako aliisaidia Yanga kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo

Metacha anastahili kupewa tuzo ya mlinda lango bora wa msimu kwa kikosi cha Yanga

2. Juma Abdul

Nahodha huyu msaidizi wa Yanga ndiye aliyekuwa mpishi mkuu wa mabao ya Yanga, akitoa pasi saba za mabao

Baada ya Mwinyi Zahera kuondolewa, aliyekuwa kocha wa muda Charles Mkwasa alimrejesha kwenye kikosi cha kwanza na baadae Luc Eymael kumfanya kuwa mchezaji muhimu wa kikosi chake

Kuimarika kwa kiwango chake, kulimpa nafasi ya kuitwa timu ya Taifa ambayo ilikwenda kushiriki michuano ya Chalenji kule Uganda

3. Jaffar Mohammed

Pamoja na kuwa hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza, Jaffar alifanya vizuri katika mechi nyingi alizotumika kama mlinzi wa kushoto

Mkwasa ndiye aliyembadilishia majukumu kutoka nafasi ya kiungo wa ushambuliaji na kumrudisha beki wa kushoto kutokana na mapungufu yaliyopo

Yeye pamoja na Adeyum Saleh walikuwa wakipokezana nafasi hiyo, lakini Jaffar alikuwa bora zaidi hasa timu inapokuwa inashambulia

4. Said Juma Makapu

Pamoja na Mwinyi Zahera kusajili walinzi wengi wa kati, ukimtoa Lamine Moro, hakuna mwingine aliyeweza kufanya vizuri zaidi ya Makapu

Makapu ameonyesha ujasiri mkubwa wakati wa Eymael, alimfanya kocha huyo amuamini na kwa kiasi kikubwa aliweza kufanya vizuri katika mechi alizocheza

Hakuna aliyetarajia kama Makapu atakuwa mlinzi wa kutegemewa wa kikosi cha Yanga, wengi waliamini kuwa mlinzi huyo mrefu alibaki kwa bahati mbaya kwenye kikosi cha msimu huu

Lakini kazi aliyoifanya bila shaka imewaziba midomo wote waliokuwa wakimkosoa

5. Lamine Moro

Moro alikuwa nguzo muhimu kwenye safu ya ulinzi wa Yanga. Anaweza kuwa mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi katika kikosi cha Yanga

Moro hakuachwa nje wakati wowote ambao alikuwa fit au hana kadi. Ameitumikia Yanga kwa nguvu zote na hakika ni aina ya wachezaji ambao Yanga itajivunia kuwa nao kwenye kikosi

6. Feisal Salum

Alianza msimu kwa kusuasua. Mwanzoni alikosolewa sana kuwa kiwango chake kimeshuka. Hata alipokuja kocha Luc Eymael hakumpa nafasi kwenye mechi zake za mwanzo

Lakini baadae Fei Toto akawa mchezaji tegemeo katika kikosi cha Yanga. Uwezo wake wa kucheza nafasi zote za kiungo, umewapa sababu makocha kumtumia vile walivyopenda kutegemeana na mfumo

7. Deus Kaseke

Kaseke ni mchezaji mwingine aliyezaliwa upya mwaka huu. Tangu ligi iliporejea baada ya mapumziko ya corona, Kaseke alikuwa chachu ya mafanikio ya Yanga. Alifunga, alitengeneza nafasi lakini pia uwezo wake wa kucheza nafasi zaidi ya moja uwanjani, uliwapa makocha uhuru wa kumtumia popote penye mapungufu

Ndio maana kuna wakati alitumika kama mlinzi wa kulia, ndani ya mechi pia alibadilishiwa majukumu kadiri alivyohitajika

8. Haruna Niyonzima

Niyonzima alipotua Yanga mwezi Januari aliongeza ubunifu kwenye safu ya kiungo. Pamoja na mapungufu yaliyokuwepo awali, timu haikuwa na kiongozi zaidi ya Papy Tshishimbi kwenye sehemu ya kiungo. Ujio wake uliisaidia hata Yanga kubadili aina ya uchezaji akifiti moja kwa moja kwenye mfumo wa Eymael

9. David Molinga

Pamoja na ukosoaji mwingi kutoka kwa mashabiki, Molinga anabaki kuwa mshambuliaji bora wa Yanga msimu huu uliomalizika

Mabao yake 11 aliyofunga kwenye ligi yameisaidia Yanga kuweza kumaliza katika nafasi ya pili

Molinga alikuwa bora miongoni mwa washambuliaji waliopo

10. Mapinduzi Balama

Balama ni mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri sana kwenye kikosi cha Yanga msimu huu. Alikuwa mtu muhimu sana kwenye safu ya kiungo na hata alipoumia, pengo lake lilionekana dhahiri. Balama anastahili kuingia kwenye kikosi bora cha Yanga msimu huu

11. Patrick Sibomana

Wakati wa Zahera, Sibomana ndiye aliyekuwa mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Yanga. Alikuwa na mchango mkubwa wakati timu ikishiriki michuano ya ligi ya mabingwa

Ni mmoja wa wachezaji ambao waliathirika na mabadiliko ya benchi la ufundi. Baada ya ujio wa Eymael hakuwa akipata nafasi mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza

Na haikushangaza kuonekana ameshuka kiwango, na kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wana nafasi ndogo ya kuendelea kubaki katika kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria

Anashika nafasi ya pili katika kupachika mabao msimu huu nyuma ya David Molinga akifunga mabao sita kwenye ligi

NYOTA WENGINE

Papy Tshishimbi

Nahodha Papy Tshishimbi amefanya vizuri kwa nyakati toafuti. Kuna wakati alikuwa nguzo muhimu katika kikosi na kuwa wakati alionekana kushuka kiwango

Hata hivyo majeraha aliyopata baada ya mapumziko ya corona, yamemfanya ashindwe kurejea kikosini licha ya kupata nafasi kwenye mchezo wa FA dhidi ya Simba

Kelvin Yondani

Mkongwe huyu nae alikuwa na mchango mkubwa msimu huu. Kwa mara ya kwanza mashabiki wamemshuhudia nohodha huyo wa zamani akitumika kama mchezaji wa kiungo katika baadhi ya mechi. Pamoja na umri wake kumtupa mkono, uzoefu wake uliisaidia Yanga kufanya vizuri katika nyakati ngumu

Abdulaziz Makame

Ni mchezaji aliyeingia na kutoka kwenye kikosi cha kwanza kwa nyakati tofauti. Hakuna shaka na kipaji chake lakini hakupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ushishani uliokuwepo katika nafasi anayocheza

Mohammed Issa 'Banka'

Banka alianza msimu vizuri akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo kwenye kikosi cha kwanza. Hata hivyo majeraha ya mara kwa mara ni kama yaliharibu mwendelezo wake kutoka mechi moja kwenda nyingine. Inaelezwa, Banka yuko mbioni kujiunga na Azam Fc

Farouk Shikhalo

Shikhalo ameonyesha kuwa mlinda lango mzuri lakini makosa aliyokuwa akifanya kwenye baadhi ya michezo yalimfanya akose kuaminiwa na benchi la ufundi

Alirejea vizuri kwenye mechi za mwisho kumaliza msimu kabla ya kupata majeraha ambayo aylimfanya akose baadhi ya michezo

Ditram Nchimbi

Pamoja na kuwa kasi yake ya kupachika mabao haikuwa nzuri, Nchimbi aliongeza kitu kwenye safu ya ushambuliaji

Wakati mwingine Eymael alimtumia kama winga na alifanya vizuri

Mrisho Ngasa

Ngasa hakuwa akivuma, lakini ni miongoni mwa wachezaji waliofanya vizuri msimu huu. Hakuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza lakini mchango wake ulionekana katika mechi alizoaminiwa

Tariq Seif

Mashabiki walikuwa na matumaini makubwa kwake na alinza vizuri majukumu yake Yanga. Amemaliza msimu akiwa na mabao matatu. Hakuwa akiaminiwa sana na benchi la ufundi, pengine kama angepewa nafasi, angefanya vizuri zaidi

Erick Kabamba

Huyu alitua usajili wa dirisha dogo. Wachezaji wenzake walikuwa wakimkubali sana lakini nae hakubahatika kuaminiwa sana na benchi la ufundi ingawa kila alipopewa nafasi alionyesha kuwa na kitu mguuni. Kama atabakishwa kwenye kikosi pengine anaweza kuwa bora zaidi msimu ujao

WALIOBORONGA!

Yikpe Gnamien

Moja ya wachezaji ambao mashabiki hawakumkubali kabisa. Hakuonyesha uwezo, huyu utakuwa muujiza kama ataendelea kubaki kwenye kikosi cha Yanga

Bernard Morrison

Aliingia kwa makeke na hakika alikuwa tumaini jipya ndani ya Yanga. Lakini kuwa mchezaji mzuri bila ya nidhamu ni kazi bure.

Leo hii hakuna shabiki mwenye muda wa kumjadili licha ya kuwa ni mchezaji ambaye mwanzoni alikuwa kwenye midomo ya kila shabiki

Huyu kajiharibia mwenyewe kutokana na nidhamu yake mbovu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’