Mabosi Yanga wakuna vichwa kusuka benchi la Ufundi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Jul 2020
Mabosi Yanga wakuna vichwa kusuka benchi la Ufundi

Mambo yanaendelea kupamba moto viunga vya Jangwani! Baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kumtimua aliyekuwa kocha wake Luc Eymael kutokana na kauli zake za kibaguzi, CV za makocha kibao zimeendelea kumiminika wakiomba kumrithi Mbelgiji huyo

Ikumbukwe pia, hata kabla ya Eymael kutimuliwa, Yanga ilikuwa na mchakato wa kusaka kocha msaidizi ambapo inaelezwa kocha huyo ameshapatikana na pengine anaweza kutangazwa wiki hii

Hitimana Thiery, Mkufunzi wa Namungo Fc anatajwa kuwa ndiye atakayekuwa kocha msaidizi wa Yanga

Klabu ya Namungo iko kwenye hatua za mwisho kumalizana na kocha kutoka DR Congo ambaye anatajwa kuja kuchukua nafasi ya Hitimana

Mnyarwanda huyo aligoma kuongeza mkataba mpya na vijana hao kutoka Ruangwa kule mkoani Lindi

Pamoja na kuwa mwenyewe (Hitimana) amekataa kata kata kuthibitisha kuwa anaelekea Yanga, lakini ni wazi jambo hilo huenda linasubiri muda mwafaka likamilishwe

Aidha katika orodha ya makocha walioomba kuinoa Yanga, inaelezwa kuwa yapo majina ya makocha kama Patrick Aussems, Hans Van Pluijm na George Lwandamina kutoka Zambia

Pluijm na Lwandamina ni makocha waliowahi kufanya kazi pamoja kwa kipindi kifupi Yanga kabla ya Pluijm kutimkia Singida United

Lwandamina alichukua nafasi ya Pluijm, wakati Mholanzi huyo akipewa cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi, cheo ambacho hakudumu nacho na hata alipoondoka Yanga wakakifuta

CV za makocha hao zinajieleza, wote waliisaidia Yanga kutwaa ubingwa wa ligi kuu na kushiriki hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho

Pluijm yeye aliipa Yanga mataji matatu ya ligi kuu huku mafanikio makubwa zaidi akiyapata msimu wa 2015/16 kwa kushinda mataji yote ya ndani

Aussems itakuwa mara yake ya kwanza kuitumikia Yanga kama ikitokea mabingwa hao wa kihistoria watamteua yeye

Lakini alijijengea heshima kubwa wakati akiinoa klabu ya Simba kwa kuisaidia timu hiyo kucheza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwaka juzi

Tangu aondoke hapa nchini, inaelezwa Aussems hakuna na timu hivyo ni kazi ambayo kama ataipata, ataifanya kwa moyo wake wote

Mashabiki wa Yanga wanasubiri kufahamu viongozi wao watamleta kocha yupi ambaye ataweza kutimiza malengo ya kushinda ubingwa wa ligi kuu msimu ujao

Mchakato huo utakamilishwa kabla ya August 14, tarehe ambayo Yanga huenda itaanza maandalizi kwa ajili ya msimu wa 2020/21

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
4h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
8h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
12h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
13h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’