Uwanja wa Uhuru chanzo cha majeruhi mengi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Nov 2017
Uwanja wa Uhuru chanzo cha majeruhi mengi Yanga
Uwanja wa Uhuru umekuwa ukilalamikiwa si na Yanga tu bali hata timu nyingine zinazoutumia uwanja huo kuwa sehemu yake ya kuchezea 'pitch' ni ngumu sana na ni chanzo cha majeruhu ya mara kwa mara.

Bahati mbaya kwa upande wa Yanga huo ndio uwanja wake wa mazoezi.

Uwanja huo umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa majeraha ya mara kwa mara ya wachezaji wa kikosi cha Yanga.

Thabani Kamusoko ni mmoja wa waathirika wa madhara ya uwanja wa Uhuru. Cjanzo cha majeraha yake ni uwanja huo.

Daktari wa Yanga Dk Edward Bavu alilazimika kumbadilishia aina ya viatu vya mazoezi kiungo huyo ambaye ni nahodha msaidizi wa kikosi cha Yanga.

Juzi kiungo Papi Tashishimbi naye alipata majeraha ambayo kulingana na Dk Bavu yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na 'pitch' ngumu ya uwanja wa Uhuru.

Tshishimbi ndio kwanza alikuwa amerejea dimbani akitokea kuugua malaria yaliyomuweka nje kwa siku tatu.

Vilabu vya Yanga na Simba viiombe Serikali iviruhusu kutumia uwanja wa Taifa ambao ukarabati wake umeshakamilika na unatarajiwa kufunguliwa rasmi wiki ijayo.

Pia viiombe kampuni ya SportPesa ambaye ndiye mdhamini wao kwa kushirikiana na Serikali kuufanyia ukarabati uwanja wa Uhuru kama walivyofanya kwenye uwanja Mkuu wa Taifa.

Aidha kama italazimu kutafuta uwanja mwingine wa mazoezi kwa klabu ya Yanga kabla ukarabati wa uwanja wa Kaunda haujakamilika ni bora kufanya hivyo.

Majeruhu ya mara kwa mara yanaathiri mwendelezo wa mafanikio ya timu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’