Mkwasa afunguka baada ya Eymael kutimuliwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2020
Mkwasa afunguka baada ya Eymael kutimuliwa

Kocha Msaidizi wa Yanga Charles Mkwasa amesema aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Luc Eymael alikuwa na mapungufu mengi ya kiutendaji na pengine kama yangefahamika mapema, asingeweza kudumu kwa muda aliokaa Yanga

Akizungumza kwa mara ya kwanza baada ya Yanga kutangaza kumfuta kazi Eymael, Mkwasa amesema kitendo alichofanya kocha huyo hakikuwa cha kiungwana na ulikuwa ni mwendelezo wa matukio yake mengi ya utovu wa nidhamu

"Eymael hakuwa mstaarabu, kashfa, dharau na lugha za matusi ilikuwa sehemu ya maisha yake, mambo hayo hayakuwa yakifahamika nje lakini juzi nadhani kila mmoja amebaini alikuwa ni mtu wa aina gani," alisema Mkwasa

Aidha akizungumzia mtafaruku uliojitokeza baina yake na kocha huyo, Mkwasa amesema aliamua kujiweka pembeni yeye mwenyewe baada ya kumsikia kocha huyo akisema hataki kufanya nae kazi

"Wakati nilipoambiwa niwe kocha msaidizi, nilikubali kwa kuwa nilidhani nitajifunza mambo mengi kutoka kwake. Lakini baada ya kufanya nae kazi nikabaini ni kocha mwenye uwezo mdogo sana.

"Mimi nilijaribu kutimiza majukumu yangu ya kumsaidia ili aweze kufanikiwa lakini ikafika wakati akaona kama namfundisha kazi. Hivyo alipotoa kauli kuwa hataki kufanya kazi na mimi na kuwataka viongozi wachague kati ya mimi au yeye, kuepusha mgogoro mimi mwenyewe nikaomba nikae pembeni"

"Mkataba wangu unamalizika mwezi wa nane, sijafahamu mipango ya Yanga lakini kwa sasa siko tayari kuwa kocha msaidizi tena. Kwani wakati mwingine unaweza kufanya kazi na makocha ambao umewazidi uwezo na kusababisha migogoro isiyokuwa na ulazima wowote" aliongeza Mkwasa

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’