Kocha wa zamani wa Yanga Mwinyi Zahera ameelezwa kushangazwa na kauli zilizotolewa na Luc Eymael, kocha aliyetimuliwa na Yanga jana baada ya kutoa kauli za kibaguzi dhidi ya mashabiki wa soka nchini
Akizungumza kwa uchungu, Zahera amesema anashangazwa na kiburi kinachoonyeshwa na kocha huyo kwani anafahamu fedha anazolipwa hapa nchini hawezi kuzipata akirudi kwao barani Ulaya
"Nimesikitika na nilipata hasira sana nliposikia sauti ya kocha akizungumza maneno mabaya. Huyo kocha amefanya makosa makubwa mawili. Kwanza pale walipocheza nyumbani kabla ya kwenda Morogoro alikwenda kusema kwamba hawataki makocha wasaidizi waliopo ama waondoke au aondoke yeye"
"Huwezi kufanya hivyo kwa sababu hilo ni suala la kuongea na uongozi ndani kisha mambo yakaisha na sio kuzungumza tena mbele ya waandishi wa habari," alisema Zahera
"Lakini pia hawa makocha wazungu hawana thamani yoyote wakirudi huku Ulaya. Hawezi kupata fedha hata dola moja, Ulaya huyu kocha hawezi kupata kazi ni mtu ambaye anafanya mambo mengi ya ajabu na inaniuma kwa sababu wazungu wengi Ulaya hawana kazi anapata bahati ya kupata dola elfu sita au elfu saba Ulaya hawezi kupata hata dola efu mbili"
"Haiwezekani kocha wa mpira aseme mambo mengi ambayo ameyasema kupitia kwenye vyombo vya habari, analalamika vitu vingi mara nyumba mara Wi-fi inaonakena kwamba ni maskini hawezi kulalamika vitu kama hivyo," aliongeza Zahera
Wadau wa soka nchini wameupongeza uongozi wa Yanga kwa kuchukua hatua haraka baada ya matamshi yake aliyoyatoa mkoani Iringa
Kocha huyo ametakiwa kuondoka nchini haraka huku TFF ikitangaza kwenda kumshitaki FIFA kwamatamshi yake ya kibaguzi aliyoyatoa dhidi ya mashabiki wa Yanga