Aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amewaomba radhi viongozi, wadhamini, mashabiki na wadau wa soka nchini kutokana na matamshi aliyotoa jana baada ya mchezo wa kukamilisha msimu dhidi ya Lipuli Fc
Eymael amedai kuwa alitoa matamshi hayo kutokana na majonzi na uchungu baada ya timu yake kumaliza nafasi ya pili
"Ningependa kuomba msamaha kwa Watanzania wote, mashabiki na wadhamini na viongozi wote wa Yanga kwa maneno yaliyotoka kinywani mwangu"
"Hayo maneno licha ya kutoka kinywani mwangu sio maneno ya Luc Eymael, hayo ni maneno yaliyotokana na kukata tamaa baada ya kumaliza katika nafasi ya pili
Nisamehe sana," Eymael alisema
Tayari Yanga imetangaza kumfuta kazi baada ya hapo jana kutoa kauli za kibaguzi na zisizo za kiungwana
ADVERTISE HERE