Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amesema amewaandaa vijana wake kuhakikisha wanaondoka na ushindi kwenye mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Jumapili, Novemba 19.
Lwandamina amesema anaiheshimu timu ya Mbeya City kwa kuwa ni moja ya timu bora msimu huu lakini hakuna namna ya wao kuepuka kipigo Jumapili.
Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kujiweka kwenye nafasi za juu katika mbio za ubingwa msimu huu.
Ikumbukwe Yanga imetoka sare michezo miwili mfululizo dhidi ya Simba na Singida United, bila shaka kipigo au sare ya tatu mfululizo ni matokeo ambayo hayatafurahiwa na mashabiki wenye shauku ya kuona timu yao inafanya vizuri kwenye kila mchezo.

ADVERTISE HERE