Bao pekee lililofungwa na mshambuliaji David Molinga limeihakikishia Yanga kumaliza ligi kuu msimu wa 2019-20 katika nafasi ya pili baada ya kuichapa Lipuli Fc bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Samora
Yanga imefikisha alama 72 ikiipiku Azam Fc ambayo ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Prisons na kufikisha alama 70
Kipigo hicho kimeishusha daraja Lipuli Fc ambayo imeungana na Ndanda Fc, Alliance na Singida United ambayo ilikuwa ya kwanza kuteremka daraja
Aidha, Mbeya City na Mbao Fc zenyewe zitacheza play-off dhidi ya timu kutoka ligi daraja la kwanza
Ulikuwa ni msimu wenye milima na mabonde kwa Yanga, lakini angalau vijana wa kocha Luc Eymael wametimiza ahadi kwa kumaliza katika nafasi ya pili baada ya kukosa ubingwa
ADVERTISE HERE