Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said amesema wamekusudia kujenga Yanga imara katika kipindi cha muda mfupi ujao
GSM wamegharamia mchakato wa Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji, Hersi anaamini kuwa mchakato huo unapaswa kukamilishwa haraka ili kuwa na timu itakayopata mafanikio yanayotarajiwa
"Kuna kanuni tatu za kufanikiwa katika uendeshaji wa timu ya mpira wa miguu, moja ni Uongozi sahihi, pili ni benchi bora la Ufundi na tatu ni kuwa na wachezaji bora. Katika kufikia malengo yetu, tunalazimika kujenga maeneo haya matatu kwa UMAKINI, UWELEDI, UZALENDO na MAPENZI MEMA kwa klabu yetu," aliandika Hersi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
"Aidha, ujenzi huu utafanyika katika muda mfupi tulionao bila kusita wala kutetereka.Hesabu siku kuanzia sasa katika safari hii itakayo wavutia sasa na hata vizazi vyetu hapo kesho," aliongeza Hersi
Tayari wataalamu wa La Liga na klabu ya Sevilla wameanza kutekeleza majukumu yao wakishirikiana na Kamati Maalum ya Mabadiliko Yanga