Kikosi cha Yanga kimeondoka mapema leo mkoani Morogoro kuelekea Iringa tayari kwa mchezo wa mwisho wa kukamilisha msimu dhidi ya Lipuli Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumapili, uwanja wa CCM Samora
Huo utakuwa mchezo muhimu sana kwa Yanga kuhakikisha wanamaliza msimu kwa heshima
Pamoja na kuwa wameondolewa kwenye nafasi ya pili na Azam Fc hapo jana, matokeo ya ushindi yanaweza kuwarejesha katika nafasi hiyo kama Azam Fc itashindwa kuibuka na ushindi dhidi ya Tanzania Prisons
ADVERTISE HERE