Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Fredrick Lugano Mwakalebela amekana tuhuma za kuihujumu klabu hiyo baada ya makomandoo wa Yanga kudai kuwa kiongozi huyo amebook hotel huko Iringa ambayo huwa inatumiwa pia na Lipuli FC.
Mwakalebela amedai kushangazwa na tuhuma hizo akibainisha kuwa tangu Jumanne alikuwa huko Kilolo akimuuguza Mama yake
Akizungumza kwa uchungu, kiongozi huyo amewaambia wanaotoa tuhumza hizo waseme kama wamemchoka ili aachie nafasi hiyo kwa amani kwani kila baya ndani ya Yanga lazima yeye (Mwakalebela) ahusishwe.
"Yaani leo kwa kweli nimesikitika sana mpaka naamua kusema maneno haya na naongea huku nikitoa machozi mimi nimekuwa nikisemwa maneno mengi, lakini naamua kukaa kimya ili kuleta amani na usalama.
"Mimi nimekwenda Iringa tangu Jumanne iliyopita kwa ajili ya kumuuguza mama yangu yupo Kilole kituo cha amani centre, baada ya hapo nimerudi na mama nyumbani nimekaa jana.
"Leo nafika Dar es Salaam naamibiwa nimebook hotel, hotel nataka kuhijumu Yanga hiyo hotel wanayoizungumzia wamebook watu wa ofsini hawajawahi kunipigia simu wala kuniambi lolote kuhusiana na hotel inapofikia timu.
"Naambiwa leo Mwakalebela anahijumu Yanga timu inaenda hotel ambayo ni ya Lipuli jamani naomba kama tumechokana niache uongozi kwa kweli naomba niwachie kwa amani kila linalokuwa baya ni Mwakalebela hivi mimi nina nguvu gani kwenye Yanga kufanya hivyo?" alihoji Mwakalebela