Ni wazi beki Andrew Vicent Chikupe hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao baada ya beki huyo 'kujiondoa' kikosini kimya kimya
Tangu amalize mgomo na kurejeshwa kikosini mwezi Janury, Chikupe amekosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza
Kocha Mkuu wa Yanga Luc Eymael amesema hafahamu alipo mchezaji huyo kwani hajamuona mazoezini kwa wiki kadhaa
"Sifahamu alipo kwani hata mazoezini simuoni, kawaulize viongozi labda wanaweza kufahamu ana matatizo yake," alisema Eymael wakati kikosi chake kikijiandaa kuelekea mkoani Iringa kukamilisha msimu kwa kuivaa Lipuli Fc
Mkataba wa Chikupe na Yanga ulishamalizika, alikuwa kwenye kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria kutimiza wajibu kulingana na maelekezo yaliyotolewa na FIFA baada ya janga la corona kuwa mikataba ya wachezaji ambayo ilikuwa ikimalizika wakati ligi zilipokuwa zimesimama kutokana na corona, inapaswa kuendelea mpaka mwishoni mwa msimu